A Vision for Change |
“Watanzania wameweka matumaini yao
kwa Chama cha CUF na misingi yake ya sera ya kuleta “Haki sawa kwa wananchi
wote” na “Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa
wote.” Chama chetu kimekuwa ni Chama kikuu cha upinzani nchini kwa muda mrefu
sasa na wananchi wanaendelea kuteseka kwa kuona matatizo yao yakizidi
kuongezeka bila kuchukuliwa kwa hatua za msingi kushughulikia matatizo yao.
Hali hii inawafanya wananchi wengi hasa vijana na wanawake kuwa katika shauku
kubwa ya kuona utawala wa nchi yetu unabadilishwa kwa amani kupitia karatasi za
kura. CUF kwa kutambua nafasi yake katika kuyaongoza Mabadiliko yanayohitajika,
kikiwa siyo tu chama kikuu cha upinzani hapa nchini bali pia kutokana na
mjengeko wake wa kuwa kweli ni chama cha kitaifa chenye kukubalika na chenye
mtandao mpana katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano, imezindua DIRA YA
MABADILIKO – VISION FOR CHANGE. Dira ya Mabadiliko ndiyo msingi wa ILANI yetu
ya uchaguzi. Vision for Change chini ya Serikali ya CUF itatujengea Tanzania
Mpya inayojali haki sawa kwa wananchi wote na itakayojenga uchumi imara
unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote.” Kwa kuisoma Manifesto
yetu ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa mwaka 2010, unaweza
kupakuwa kwenye kiungo hapo chini.
CUF Manifesto 2010
No comments:
Post a Comment