Sunday, November 25, 2012

MSIMAMO WA JUMUIYA YA VIJANA KWA TFDA NA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.

Naibu katibu Mkuu JUVICF-Thomas Malima

 TFDA ibomolewe, isukwe upya, wahujumu wa madawa ya umma washitakiwe.
Vinara wa Madawa ya kulevya nao watajwe na kufikishwa mahakamani.
Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Dawa, pamoja na Mamlaka ya Bandari vimekuwa mawakala wakubwa wa biashara haramu ya afya za watanzania. Afya za watanzania zinaendelea kuwekwa rehani na waliopewa mamlaka ya kuongoza.
Wizara ya Afya imekuwa ikiruhusu uwepo wa zahanati na maduka ya madawa yasiyo na wataalamu wa afya ambapo watanzania wengi wamekuwa wakipewa dawa zisiendana na magonjwa wanayoumwa. Hali imesababisha madhara makubwa kwa wagonjwa. Utafiti uliofanywa na Youth Initiative Tanzania (yiTa) na TWAWEZA kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012 ulibaini kuwa zaidi ya 93% ya huduma zinazotolewa katika zahanati na maduka binafsi ya dawa jijini Dar es salaam, hutolewa bila kutumia utaalamu wa afya. Je, wizara ya Afya ina mpango gani wa kukomesha hali hii?.
Pamoja na hali kuwa mbaya kiasi hicho, TFDA imekuwa ikpata kashfa kubwa za kuhatariasha maisha ya watu kila kukicha lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya mabosi wa TFDA. Watanzania watakumbuka kuwa mwishoni mwa mwaka 2011 watafiti wa ugonjwa wa Maralia toka Uingereza wakiongozwa na Dr. Washington walitoa ripoti juu namna ambavyo Serikali za Afrika zimekuwa zikipokea madawa bandia toka China na namna ambavyo madawa hayo yanavyoathiri afya za watu. Lakin cha ajabu TFDA ilikana kupokea madawa bandia, lakini baada ya miezi miwili madawa bandia ya Maralia yakakamatwa Mwanza na Kilimanjaro. Ndipo baadaye viongozi wa TFDA walipojitokeza kwa aibu na kukiri kuwapo kwa madawa hayo bandia nchini. Lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao.
Hivi karibuni, kumepatika dawa feki za kuongeza nguvu za waathirika wa VVU, lakini pia hakuna hatua zozote zilizokwisha chukuliwa.
Na cha kusikitisha zaidi, ni pale Watanzania wanaambiwa kuwa hakuna dawa katika hospitali za umma wakati hospitali za binafsi zina shehena ya dawa zilizoandikwa “NOT FOR SALE”. Na cha ajabu zaidi TFDA wanakili kuwa wameibiwa dawa zilizotakiwa zitolewe bure kwenye zahanati na hospitali za serikali lakini zimepotea na zinapatikana katika hospitali na maduka binafsi ya dawa zikiwa zimefutwa nembo ya NOT FOR SALE. Wakati haya yanatendeka, hospitali za umma ziko taabani, hakuna dawa. Imebaki kwenda hospitali na kupima, kisha unaambiwa nenda ukanunue dawa katika dawa Fulani. Lakini serikali imekaa kimya dhiti ya mamlaka hizi.
Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF), inatambua kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, kunahatri kubwa ya kuwapoteza watoto wengi ambao ndio vijana wa kesho. Akina mama na Vijana nao wako hatarini kupotea. Hivyo tunaitaka serikali kuwaachisha kazi wakurugenzi wote wa TFDA ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Nalo suala la watuhumiwa wa madawa ya kulevya limewekwa kwapuni kwa sasa. Serikali ilishahidi kutoa orodha yao lakini haitaki kutoa hadi sasa. Hili ni suala linaloathiri maisha na nguvu kazi ya vijana moja kwa moja. Vijana wengi wanapotea kwa kuathirika na madawa ya kulevya.
JUVICUF inaitaka serikali iwataje wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya nchini bila kujali vyeo na haiba yao katika jamii. Na baada ya kuwataja, wafikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Endapo serikali haitachukua hatua za kuisafisha TFDA na kuwataja pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa madawa ya kulevya kama ilivyoahidi, na kwa kuwa waathirika wakubwa madawa ya Kulevya na madhara ya kuuzwa kwa dawa kiholela pamoja hospitali za umma kukosa dawa ni Vijana, JUVICUF itafanya maandamano ya amani hadi wizara ya afya kushinikiza hatua za uwajibikaji na kisheria zichukuliwe.
Imeandaliwa na:
Thomas D.C Malima
Naibu Katibu
Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF)-Taifa.

Tuesday, November 6, 2012

MWANDISHI HUYU HANA AKILI TIMAMU?

SOMA MAKALA YAKE YENYE KICHWA CHA HABARI
PROFESSA LIPUMBA NI MBUMBUMBU WA SHERIA,ACHA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE
NA HAPPINESS KATABAZI
KWA mara ya pili sasa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba  amekuwa akiitisha mikutano na waandishi wa habari kuzungumzia vurugu za kidini zilizotokea hapa nchini hususani jijini Dar es Salaam.
Profesa Lipumba pamoja na mambo mengine amekuwa akisema tena kwa ujasiri kuwa kesi ya jinai namba 245/2012 inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49 iliyofunguliwa na upande wa jamhuri Oktoba 18 mwaka huu, ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Victoria Nongwa na inendwa na wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka wakati upande wa utetezi unatetewa na wakili wa kujitegemea Mansoor Nassor ilipaswa iwe ya madai na siyo jinai na kwamba eti Ponda alistahili dhamana na kuwa anafanya mpango wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete amshauri serikali ifanye mazungumzo na Maimamu wa misikiti ili waweze kupata suluhu ya tatizo la vurugu hizo za kidini.
Binafsi ni mwandishi wa habari za mahakamani hapa nchini na kesi hii ni miongoni mwa kesi ambazo minaziudhulia siku ilipofunguliwa kwa mara ya kwanza ,na hata  Novemba Mosi mwaka huu,kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa na wakili wa serikali Kweka aliieleza mahakama kuwa uplelezi wa shauri hilo umekamilika nilikuwepo tangu saa moja asubuhi mahakamani hapo, na  hata hiyo  Novemba 15 mwaka huu, panapo majaliwa ya mwenyezi mungu kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya upane wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa nitakuwepo ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo kwaajili ya kuiripoti kesi hiyo kwa uweledi wa aina yake.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ya kesi hiyo inayomkabili Ponda na wenzake ambayo nakala yake ninayo, ina jumla ya mshitaka matano ambapo mashitaka yote matano yanamkabili Ponda na mashitaka manne yanamkabili mshitakiwa 2-50.
Kosa la kwanza  ni la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu cha  384 cha Sheri ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa wote wanaidaiwa kuwa Oktoba 12 mwaka huu katika eneo la Chang’ombe  Marksi walikula njama kwania ya kutenda kosa.Kosa la pili ni  kuingia kwa nguvu  kwa nia ya kutenda kosa  kinyume na kifungu  cha 85,35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ,kuwa Oktoba 12 mwaka huu,  katika eneo la Chang’ombe Markasi ,kwa jinai na wasipokuwa na sababu  waliingia kwenye kiwanja cha eneo hilo kinachomilikiwa na Kiwanda cha Agritanza.
Wakati kosa la tatu ni  la kujimilikisha kwa jinai kiwanja hicho kinyume na kifungu cha 86 na 35 cha Sheria hiyo  kuwa kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu, katika eneo hilo pasipo na uhalali washitakiwa wote  katika hali ya kupelekea uvunjifu wa amani,walijimilikisha  kwa nguvu ardhi ya kampuni ya Agritanza.
Shitaka la nne ni la wizi kinyume na kifungu cha 258 na 225 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu  ya mwaka 2002  kuwa washitakiwa wote kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu, waliiba vifaa,malighafi  kama nondo,matofali ,kokoto zenye jumla ya Sh 59,650,000 mali ya Kampuni hiyo.
Aidha shitaka la tano ni kwaajili ya Ponda peke yake ambalo ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni  ya Adhabu  ya mwaka 2002 kuwa Oktoba 12 katika eneo hilo la Chang’ombe  kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu  aliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao watende makosa hayo.Na washitakiwa wote walikanusha mashitaka hayo na Hakimu Nongwa akasema mashitaka yote yanadhamana kwa mujibu wa sheria na akatoa masharti ya dhamana kwa mshitakiwa 2-50 .
Na kusema ili wapate dhamana nilazima kila mmoja awe na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini bondi ya milioni moja, licha Hakimu Nongwa alisema mahakama yake haiwezi kutoa dhamana kwa Ponda licha anastahili dhamana kwasababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kufunga dhamana ya Ponda kwa mujibu wa kifungu cha 148(4) cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.Na hati hiyo ya DPP inakuwa imeifunga mikono mahakama hadi hapo siku DPP atakapoona haja ya kuiondoa hati hiyo hivyo Ponda ataendelea kusota rumande hadi hati hiyo itakapoondolewa na DPP .
Kauli ya Profesa Lipumba kuhusu kesi ya Ponda imenifanya nianze kuamini kuwa hata ukiwa msomi wa hali ya juu kama Profesa Lipumba unaweza pia kutoa maoni ya kipuuzi ambayo hayapaswi kutolewa na msomi wa aina yake mbele ya umma.
Tumuulize huyu Lipumba kabla ya kutoa kauli hizo aliwasiliana na wanasheria wa chama chake wakampa ushauri wa kisheria wa nini cha kuzungumza mbele ya umma kuhusu kesi ya Ponda inayooendelea pale katika Mahakama ya Kisutu?Naamini hakupata ushauri  mzuri toka kwa wanasheria wa chama chake au kama alipata basi wanasheria huo waliamua kumpatia ushauri ambao umemdhalilisha Lipumba mbele ya jamii ya wasomi wa sheria na jamii inayoheshimu utawala wa sheria hapa nchini.
Profesa Lipumba kwanza kabla ya kutoa kauli hizo kuhusu kesi ya Sheikh Ponda kuwa kesi hiyo ya jinai namba 245 /2010 eti ilipaswa iwe ya jinai, ungeitafuta hati hati ya mashitaka ungeisoma vizuri na ungeweza kuelewa makosa wanayoshtakiwa nayo ni ya madai au jinai  halafu ungeenda kuisoma Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code;2002),Sheria ya Mashauri ya Madai(Civil Procedure Code:2002) na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act, RE:2002) na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naamini vingekupa mwongozo mzuri sana kwa kufahamu mashitaka yanayowakabili, kifungu gani kimetumika kufunga dhamana ya Ponda na ni kwanini dhamana yake imefungwa na pia ungeweza kufahamu vyema majukumu ya mahakama ni ya pili nay a serikali ni yapi.
Na hapo ndipo ninapokubaliana na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa wiki  ambayo inawataka wanasiasa waache unafki kwani wao wanaisasa wanaishi maisha kifahali na uhuru wakati wale wafuasi wao wanaishi maisha ya tabu na wamekuwa wakiwapandikisha uongo wafuasi wao.
Sasa kwa kauli hiyo ya Kikwete minaona katika matamko hayo ya Lipumba inamgusa pia, kwani uenda Lipumba anataka kujipatia umaarufu chee wa kisiasa kupitia kesi ya Ponda ila hafahamu kuwa mahakama haiendeshwi wala haisikilizi kauliza wanasiasa  pindi inapofanyakazi zake kwa mujibu wa sheria.
Wewe Lipumba kwakuwa unasema kesi ya jinai ya Ponda ilipaswa iwe ni ya madai, hivi ni kwanini unashindwa kuomba kazi ya kuwatetea washitakiwa hao kama (Bush Lawyer )mahakamani hapo na siku kesi ikianza kusikilizwa ukawasilisha hilo pingamizi lako lakutaka kesi hiyo ya jinai ifutwe kwani imefunguliwa kimakosa ilitakiwa washitakiwa hao wafunguliwe kesi ya madai).
Maana unapozungumzia kesi hiyo kwenye majukwaa na mbele ya waandishi wa habari haimsaidii Ponda kwa lolote zaidi zaidi unazidi kumgandamiza Ponda bila wewe kujua?
Profesa mzima tena wa uchumi unayeheshimika nchi mbalimbali unashindwa kufahamu mtu anayetuhumiwa kwa kosa la wizi au kuingia kwa nguvu kwenye kiwanja au chochezi basi mtu huyo makosa hayo yataangukia kwenye jamii ya makosa ya jinai? Lakini wewe sijui kwa upotoshaji au unalako jambo unadiriki kujitokeza adharani kuuposha umma kwa kusema walipaswa washitakiwe kwa kesi ya madai?
Mwenyekiti mzima wa chama kikubwa kama CUF,ambacho chama hicho chini ya uongozi wako ni miongoni mwa chama kilichokuwa kidai Tanzania iandike Katiba mpya kwa madai kuwa Katiba ya sasa imepitwa na wakati,na kwa maana hiyo unaifahamu vyema ibara za Katiba hiyo , unashindwa kuifahamu Katiba ya nchi ambayo Ibara ya 59B(1)  inayosomeka hivi; “Kutakuwa na Mkurugenzi wa Mashtaka  ambaye atateuliwa  na Rais,kutoka miongoni  mwa watu wenye  sifa zilizoanishwa  katika ibara ndogo (2) ya ibara  59 na amekuwa  na sifa hizo mfululizo kwa muad  usiopungua  miaka kumi.
Ibara ya 59(4) inasema; ‘Katika kutekeleza  mamlaka yake,Mkurugenzi wa Mashitaka  atakuwa huru ,hataingiliwa  na mtu yeyote  au mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo; (a) nia ya kutenda haki, kuzuia matumuzi mabaya ya taratibu  za utoaji  haki na maslahi ya umma.
Na kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai, kina mpa mamlaka DPP kufunga dhamana ya mshitakiwa na ndiyo kifungu hicho kilichotumia na DPP kufunga dhamana ya Ponda.
Ni kweli dhamana ni haki ya kila mtu ila kuna baadhi ya makosa hayana dhamana na mfano kesi ya mauji, utakatishaji fedha haramu( Money Laundry),unyang’anyi wa kutumia silaha(Amry Robbery) mauji,uhaini na ugaidi (Terrorisms)  lakini kama kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, kinampa mamlaka DPP kumfungua dhamana mshitakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika.
Sasa kwa mtiririko huo ,misimwelewi Lipumba ana ajenda gani iliyojificha kwenye hii kesi ya Ponda.Kwani Ponda na wenzake bado ni watuhumiwa kama wengine tub ado hajaukumiwa.DPP ametumia madaraka aliyonayo kufunga dhamana ya Ponda na  kuwafungulia mashitaka ya jinai washitakiwa hao ,sasa sijui tabu inatoka wapi.
Mbona viongozi wa iliyokuwa Taasisi ya Upatu (DECI) walivyofunguliwa kesi pale Mahakama ya Kisutu mwaka 2009, na makosa yanayowakabili yalikuwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria lakini  DPP huyu huyu Dk.Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungua dhamana na vigogo ambao kesi yao iliyopo mbele ya Hakimu Stewart Sanga imefikia hatua ya wao wameanza kujitetea,aliwafungia dhamana na walisota gerezani kwa zaidi ya miezi mitatu, mbona hatukuwasikia wanasiasa wala waumini wa dini ya Kikristo au wewe Lipumba na wale wafuasi wengine mnaondamana kila Ijumaa kushinikiza Ponda aachiliwe huru, hamkuandamana kushinikiza waachiliwe huru na kwamba kesi yao vigogo wa DECI ni ya madia?
Tuachane na uhuni huu unaofanywa na wasiasa waliopoteza dira na mwelekeo na waliofirisika kisiasa ambao wao masuala hatarishi na yanayoingilia uhuru wa mahakama ambao uhuru wa mahakama umeainishwa wazi katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inasomeka hivi; “Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki ,mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia  tu masharti ya Katiba na Sheria za Nchi’.
Na ibara 107A (1) ya Katiba ya nchi inasema “Mamlaka yenye mamlaka ya mwisho ya utoaji  haki katika jamhuri ya Muungano  itakuwa ni Mahakama.
Kwahiyo kama  kesi inayomkabili Ponda ni ya madai , si jukumu la wewe Lipumba sasa kusema hilo ni jukumu la Mahakama siku ikifika itasema hivyo.
Mwisho napenda kuwaasa wale wanaojiita wafuasi wanaojiita wao ni wafuasi wa  Ponda na sheikh Farid waache kushiriki kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kisingizo cha kuishinikiza serikali na mahakama imwachilie huru Ponda kwani kufanya hivyo ni wazi wakae wakijua watakuwa wanafunja sheria za nchi watajikuta wanaingia matatani na wao waishia kwa kufunguliwa kesi za jinai mahakamani na kutupwa jela.
Na wale wahuni wachache ambao ni wazi wamechoka kuishi Tanzania kwenye amani wanaoleta vurugu za kidini kwa kisingizio eti wanaitetea dini ya kiislamu, wakome mara moja na kwa uwezo wa mungu hiyo dhamira yao mbaya na kishetani ya kutaka kuingiza Tanzania kwenye machafuko haitafanikiwa nao mwisho wa siku wataambulia kipigo kutoka kwa wanausalama wetu na kufikishwa mahakamani na mwishowe kupelekwa kupumzika katika gereza la Segerea,Keko na kula ugali wa bure na kuwa chini ya ulinzi.
Naendelea kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwadhibiti wahuni hawa wachache wanajaribu kutaka kuatarisha usalama wa taifa letu kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.Na ninaviomba vyombo vya dola viwashughulikie kikamilifu wale wote wanaoleta vurugu kwa kisingizio cha kutetea dini ya kiislamu wakati bado wakristo,waislamu na wapagani hapa nchini tunaishi kwa upendo,tunafanyakazi pamoja.
Mwisho nimalizie kwa kuwataka waandishi wa habari wenzangu na wanaharakati na wanasiasa ambao huko nyuma tulikuwa mstari wa mbele sana kushikilia bango hadi kuandaa maandamano na kutengeneza mabango na fulani za kulaani tuhuma za ufisadi katika Mkataba wa Dowans,Richmond, mauji ya mwanahabari mwenzetu David Mwangosi,kufungiwa kwa vyombo mbalimbali vya habari.
Mbona wanahabari wenzangu wengi,wanaharakati,na wanasiasa machahari mbona tumeonekana kuwa wapole sana katika matukio haya yanayotaka kuleta chochoko za kidini? 
Hivi  je matukio haya yanayoashiria chokochoko ya udini siyana madhara ya haraka,wazi ambayo yasingezibitiwaharaka na vyombo vya dola na hekima ya viongozi wa dini ya Kikristo na wale wa kiislamu leo hii Tanzania ingekuwa imeingia kwenye machafuko ya kidini?
Tuache unafki,amani ni kitu muhimu sana pote pale duniani na chenye kipaumbele halafu hayo mambo mengine yanafuata.Kwani bila ya kuwepo na amani huo ufisadi usingenyika.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
0716 774494
 
 
Mwisho wa makala yake, chadema wanasemaje juu ya kadhia hiyo?
 
 

Chadema waweka bayana msimamo wao juu yaliowasibu ma-shiekh


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.
Wanasheria hao wa CHADEMA wamesema kuwa kitendo cha serikali kumnyima dhamana Sheikh Ponda ni kinyume cha katiba na kwamba Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola, hakiwezi kuvumilia kuona haki za raia zikivunjwa.
“Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini,” ameeleza Marando katika mkutano huo.
Marando alifika mbali zaidi kwa kusema tatizo lililopo sasa kati ya serikali na waislamu, limetokana na hatua ya serikali kuwalazimisha waislamu wote kuwa waumini wa Bakwata, chombo ambacho wengi wanakiona kinatumika kuwakandamiza.
Naye Profesa Safari alionya matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotumiwa na serikali kwa kisingizio cha kulinda amani, huku akieleza kuwa matumizi ya kijeshi siyo suluhu ya kutatua matatizo yaliopo.
Kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Faridi na kumzuia kwa siku tatu, wanasheria hao wamesisitiza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.
“Kitendo cha kumkamata na kumshikiria Sheikh Faridi, huku serikali na vyombo vyake vikisema havihusiki, wakati ukweli ni kuwa alikuwa anashikiliwa na watu wa USALAMA wa TAIFA, ni uharamia mkubwa unaopaswa kulaaniwa na wote wanaolitakia mema taifa hili,” ameeleza Marando.
Kuhusu uvunjwaji wa makanisa, Profesa Safari amesema CHADEMA kimelaani hatua hiyo iliyotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi. Amewataka waislamu kuvuta subira.
Hata hivyo, Profesa Safari amesena matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.
Chanzo Chadema Blog

Mwisho wa msimamo wa chadema, unaofuata ni msimamo wa cuf uliotolewa na Prof Ibrahim Haruna Lipumba.



                THE CIVIC UNITED FRONT                       (CUF –Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU JUHUDI ZA CUF ZA KUENDELEZA AMANI NA UTULIVU BAADA YA SALA YA IJUMAA TAREHE 2 NOVEMBA 2012

Siku ya Alhamis nikielekea Muhimbili kumpeleka shangazi yangu hospitali nilipata taarifa kuwa Imam wa msikiti wa Masjid Haq (ulioko jirani na Afisi Kuuya CUF na ambapo nasali sala ya Ijumaa nikiwa Afisi Kuu) na watu wengine watatu akiwemo Sheikh Ramadhan S. Sanze (ambaye namfahamu kwa muda mrefu). Sadik Gogo na Mzee Abdillah wamekamatwa na wamefikishwa kituo cha polisi cha kati (Central Police Station). Nilistushwa na kamata kamata hiina nikahofia kuwa inaweza kuongeza jazba miongoni mwa waumini wa Kiislam. Baada ya shangazi kupata tiba katika hospitali ya Muhimbili nilimrudisha nyumbani na nikampigia simu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na mahusiano ya umma, Abdul Kambaya, tukutane kituo cha polisi cha kati kuulizia sababu za kukamatwa Imam wa MasjidHaq na wenzake watatu na kama tunaweza kuwawekea dhamana.Tulipof ika kituo cha polisi tulibaini kuwa Imam wa Msikiti wa Masjid Haq hajakamatwa bali kuna muumini mwingine kwa jina la Mkadam Swalehe ndiye aliyekamatwa. Tulizungumza na RPC Kova na RCO Msangi kuhusu kuachiliwa kwa wale waliokamatwa. Tukafahamishwa kuwa itabidi wafanyiwe mahojiano na baadaye wataachiliwa isipokuwa Mkadam Swalehe ambaye ana faili jingine pale polisi linaloendelea kufanyiwa upelelezi. Tulifahamishwa kuwa nitume mtu saa 10:30 jioni ili aweze kufuatilia utaratibu wa kuachiliwa watuhumiwa watatu akiwemo Sheikh Ramadhan Sanze, Sadik Gogo na Mzee Abdillah.Nilish auriana na Wakurugenzi wa CUF walioko Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro hatua za kuchukua. Taarifa za kukamatwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake zilikuwa zinaenea na kupandisha jazba ya Waislam wengi. Tulipata wasiwasi kuwa jazba hii inaweza kupelekea Waislam wengi kuandamana baada ya sala ya Ijumaa.Ikiwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wataachiwa na Waislam wakapata taarifa hiyo inaweza kusaidia kupunguza jazba na watu wasishiriki maandamano baada ya sala ya Ijumaa.Nilimpa jukum Abdul Kambaya afuatilie Central PoliceStation, suala la kuachiliwa Sheikh Sanze na wenzake. Niliwasiliana naye kwa simu na kuzungumza na RCO na nikaamini kuwa Sheikh Ramadhan Sanze, Sadik Gogo na Mzee Abdillah wataachiwa baada ya kukamilishamaho jiano. Ilikuwa inakaribia saa 12 jioni. Muda wa kuitisha Press Conference haukuwepo. Tukakubaliana Naibu Katibu Mkuu awasiliane na wahariri wa habari wa vituo vya televisheni Channel10, TBC1, Star TV, Mlimani TV na ITV ili niweze kutoa taarifa ya kuwasihi Waislam warudi majumbani na kwenye shughuli zao baada ya sala ya Ijumaa. Niliweza kufanya mahojiano na Channel 10, TBC1, na ITV. Kwa bahati mbaya Camera person wa Star TV alikuwa kwenye shughuli nyingine na kwa hiyo sikuweza kufanya mahojiano na Star TV. Vilevile wapiga picha wa Mlimani TV hawakuwepo kwenye studio. Pia nilipatabahati ya kuzungumza na Radio Iman inayosikilizwa na Waislam wengi na kueleza maoni yangu kuwa Waislam wasiandamane baada ya sala ya Ijumaa.Baada ya kutoa taarifa kwenye vituo vitatu vya televisheni na Radio Iman kuwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wataachiliwa na kuwasihi Waislam wasishiriki maandamano baada ya sala ya Ijumaa nilimpigia simu Abdul Kambaya kuulizia kama naweza kuzungumza na Sheikh Ramadhan Sanze. Kambaya akanieleza mambo yamebadilikana hawajaachiwa. Niliwasiliana na RCOna nikabaini kuwa suala hilo haliko tena chini ya uamuzi wake na litakamilishwa siku ijayo.Usiku wa alhamisi kuamkia Ijumaa nilijaribu kuwasiliana na Rais Kikwete kupitia wasaidizi wake ili nimfahamishe mantiki na sababu ya hatua nilizochukua na atumie uwezo wake alionao Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waachiliwe. Kwa bahati msaidizi mmoja alipata ujumbe wangu wa simu na akanipigia simu saa 6:50 usiku na kunifahamisha atajitahidi kuufikisha ujumbe wangu kwa Mhe. Rais ili nipate kuongea naye kuhusu jamaa wanaoshikiliwa na polisi waachiwe ili kupunguza jazba na kuepusha shari. Niliyezungumza naye alikuwa Dodoma na Rais alikuwa Arusha na ratiba yake ilikuwa imebana sana na kwa hiyo hakuweza kupata fursa ya kunipigia simu siku hiyo ya Ijumaa.Siku ya Ijumaa Abdul Kambaya aliendelea kufuatilia kuachiwa kwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake Central Police Station. Nami katika kuhangaika ili waliokamatwa waachiliwe nilipata fursa ya kuzungumza na IGP na kumfahamisha sababu ya juhudi nilizochukua na mategemeo yangu kuwa Sheikh Sanze na wenzake wangeachiwa. Ninakiri kuwa katika mazungumzo ya simu, IGP Mwema alikuwa msikivu na mkarimu sana katika kauli yake. Alinishukuru kwa kauli niliyoitoa katika vituo vya televisheni na kuwa atafuatilia suala nililomueleza. Hatimaye Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waliachiwa.Naam ini kama Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wangeachiwa ingesaidia sana kupunguza jazba. Hata hivyo Waislam wengi na wananchi wengine kwa ujumla walipokea vizuri wito wangu na hawakushiriki katika maandamano. Baadhi wamenikosoa na kushauri kuwa ilifaa nisubiri mpaka baada ya maandamano kufanyika na kama patatokea majeruhi na vifo ndipo nitoe tamko la kulaani vitendo vya polisi na serikali.Katika mitandao ya kijamii wengine wamekejeli juhudi zangu. Nilikubali kushiriki katika kipindi cha Makutano show kinachoendeshwa na Bi. Fina ambapo hupata maswali toka Jamii Forum. Moja ya swali lililotolewa ni “Muulize very very solid, kuna agenda gani kati ya Cuf na uislam? mtaani leo wanasema kauli ya Lipumba ya jana kusitisha maandamano wameitii, na ukiangalia mikutano yake pale jangwani utafikiri kuna mawaidha ni balaghashia na baibui.” Fina hakupata muda wa kuniuliza swali hili. Jibu lake ni la wazi. CUF inasimamia Haki Sawa kwa Wananchi Wote. Kuna Watanzania wengi ambao ni Waislam na wao pia wanastahiki kutendewa haki katika nchi yao. Kuhusu balaghashia na baibui ni vyema vijana wakatazama picha za umati wa watu uliokuwa unahutubiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa nchi hii. Picha hizo pia zinaonyesha waliokuwa wakipigania uhuru wengi walivaa balaghashia na baibui hata Mwalimu Nyerere alipewa zawadi nyingi za balaghashia na akaamua kuzivaa. Kushamiri kwa demokrasia ya kweli msingi wake mkubwa ni amani na utulivu. Amani ya kweli haipatikani bila kuwepo haki. Kesi ya Sheikh Ponda msingi wake na madai ya kiwanja. Ki msingi kesi ya madai ya kusuluhishwa na Mahakama ya ardhi. Sheikh Ponda ana haki ya msingi ya kupewa dhamana hata kama kauli zake haziifurahishi serikali.Nasiki tika sana katika kipindi hiki tete,viongozi wa serikali wameshindwa kuchukua juhudi za makusudi kuzungumza na Maimam wa misikiti na viongozi wa asasi za Kiislam kupunguza jazba. Badala yake wameachia kauli za vitisho vya Kamanda Kova ndiyo viwe mawasiliano kati ya serikali na Waislam.Ni vyema serikali ikatumia busara na kuwasiliana na Maimamu wa misikiti na viongozi wa asasi za Kiislam kuelewa hoja na malalamiko yao.Hatimaye nimepata fursa ya kuzungumza na Mheshimiwa Rais leo asubuhi na nikamueleza juhudi nilizozichukua kuweza kupunguza jazba na kuwaomba Waislam wasishiriki kwenye maandamano baada ya sala ya Ijumaa. Ni wazi hali hii ya mtafaruku ndani ya jamii inamsononesha sana Mheshimiwa Rais na ninaamini atajitahidi kwa uwezo wake wote kutafuta suluhisho.Katik a kutafuta suluhu ya mtafaruku huu nitaendelea na jitihada za kutafuta fursa niweze kubadilishana mawazo na Rais Kikwete. Nitazungumza na viongozi wa asasi za Kiislam. Nitazungumza na viongozi wa Makanisa ya Kikristo. Madhumuni ya mazungumzo yangu nikuwafahamisha mantiki ya juhudi nilizofanya na kushauriana misingi muhimu ya Waumini wote kuheshimiana na kuvumiliana ili tujenge Tanzania yenye haki sawa kwa wote.

Ibrahim Haruna Lipumba

Mwenyekiti
Novemba 4 2012
 
 
KWANINI ANATUKANWA PROF LIPUMBA PEKEE? HUHU MUANDISHI NI MBUMBU AU HANA AKILI TIMAMU?, WAANDISHI WENYE UPENDELEO WA DHAHILI NDIO WALIOSABABISHA MAUAJI YA KIMBALI RWANDA NA BURUNDI. WAANDISHI TUACHE UNAFKI.

Wabunge wataka Serikali tatu

(Kifupi: WAPENDEKEZA MAWAZIRI WASIWE WABUNGE, VITI MAALUMU VIFUTWE, URAIS MIAKA 35)
WABUNGE jana walijilipua baada ya baadhi yao kupendekeza kuwa muundo wa Muungano ubadilishwe kuwa wa Serikali tatu na kwamba, mawaziri wasiwe  wabunge.
Pamoja na mapendekezo hayo, wengine walitaka umri wa kugombea urais ushushwe na kuwa miaka 35, badala ya sasa ya miaka 45.
Wakitoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba mjini Dodoma jana, wabunge hao pia walitaka viti maalumu vya ubunge vifutwe, badala yake wanawake warejee kugombea ubunge majimboni.
Katika mkutano huo, zaidi ya wabunge 36 walitumia nafasi hiyo kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali yenye masilahi kwa taifa, waliyoona yanafaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya, ambayo mchakato wa ukusanyaji maoni ya uundwaji wake, unaendelea.
Muungano
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alitaka muundo wa muungano ubadilishwe na kuwa wa Serikali tatu, badala ya uliopo sasa aliosema una kasoro nyingi.
Moja ya kasoro hiyo ni wawakilishi kuruhusiwa kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, huku wabunge wa Bara wakiwa hawana uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi.
“Mwenyekiti, tuwe na Serikali tatu katika muungano, vinginevyo kila mmoja abaki na chake," alisema.
Pia alitaka viti maalumu vifutwe, badala yake wanawake wawekewe majimbo ya wilaya, ambayo watagombea na wenzao.
Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo naye alitaka muundo wa muungano uwe wa Serikali tatu pamoja na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika  nafasi mbalimbali.
Alisema kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wasitokane na wabunge kwa sababu hawataweza kufanya kazi kwa ufanisi na ni mgongano wa kimasilahi.
Mbunge wa Mkanyangeni (CUF), Mohamed Mnyaa alitaka kuwapo na Serikali tatu katika muungano.
Alisema kama Tanzania Bara watakataa kuita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita jina lolote hata Mzizima.
“Muungano uwe wa Serikali tatu, Tanganyika wawe na nchi yao na sisi tuwe na Zanzibar yetu, kama bara hawataki kuiita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita hata Mzizima,”  alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Chakechake, (CUF), Mussa Haji Kombo alitaka muundo wa Muungano uliopo ubadilishwe badala yake uwe wa mkataba.
Chanzo: mwananchi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU JUHUDI ZA CUF ZA KUENDELEZA AMANI NA UTULIVU BAADA YA SALA YA IJUMAA TAREHE

Mwenyekiti Cuf Taifa - Prof Ibrahim Haruna Lipumba
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU JUHUDI ZA CUF ZA KUENDELEZA AMANI NA UTULIVU BAADA YA SALA YA IJUMAA TAREHE 2 NOVEMBA 2012
Siku ya Alhamis nikielekea Muhimbili kumpeleka shangazi yangu hospitali nilipata taarifa kuwa Imam wa msikiti wa Masjid Haq (ulioko jirani na Afisi Kuu ya CUF na ambapo nasali sala ya Ijumaa nikiwa Afisi Kuu) na watu wengine watatu akiwemo Sheikh Ramadhan S. Sanze (ambaye namfahamu kwa muda mrefu). Sadik Gogo na Mzee Abdillah wamekamatwa na wamefikishwa kituo cha polisi cha kati (Central Police Station). Nilistushwa na kamata kamata hii na nikahofia kuwa inaweza kuongeza jazba miongoni mwa waumini wa Kiislam. Baada ya shangazi kupata tiba katika hospitali ya Muhimbili nilimrudisha nyumbani na nikampigia simu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na mahusiano ya umma, Abdul Kambaya, tukutane kituo cha polisi cha kati kuulizia sababu za kukamatwa Imam wa Masjid Haq na wenzake watatu na kama tunaweza kuwawekea dhamana.
Tulipofika kituo cha polisi tulibaini kuwa Imam wa Msikiti wa Masjid Haq hajakamatwa bali kuna muumini mwingine kwa jina la Mkadam Swalehe ndiye aliyekamatwa. Tulizungumza na RPC Kova na RCO Msangi kuhusu kuachiliwa kwa wale waliokamatwa. Tukafahamishwa kuwa itabidi wafanyiwe mahojiano na baadaye wataachiliwa isipokuwa Mkadam Swalehe ambaye ana faili jingine pale polisi linaloendelea kufanyiwa upelelezi. Tulifahamishwa kuwa nitume mtu saa 10:30 jioni ili aweze kufuatilia utaratibu wa kuachiliwa watuhumiwa watatu akiwemo Sheikh Ramadhan Sanze, Sadik Gogo na Mzee Abdillah.
Nilishauriana na Wakurugenzi wa CUF walioko Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro hatua za kuchukua. Taarifa za kukamatwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake zilikuwa zinaenea na kupandisha jazba ya Waislam wengi. Tulipata wasiwasi kuwa jazba hii inaweza kupelekea Waislam wengi kuandamana baada ya sala ya Ijumaa. Ikiwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wataachiwa na Waislam wakapata taarifa hiyo inaweza kusaidia kupunguza jazba na watu wasishiriki maandamano baada ya sala ya Ijumaa.
Nilimpa jukum Abdul Kambaya afuatilie Central PoliceStation, suala la kuachiliwa Sheikh Sanze na wenzake. Niliwasiliana naye kwa simu na kuzungumza na RCO na nikaamini kuwa Sheikh Ramadhan Sanze, Sadik Gogo na Mzee Abdillah wataachiwa baada ya kukamilisha mahojiano. Ilikuwa inakaribia saa 12 jioni. Muda wa kuitisha Press Conference haukuwepo. Tukakubaliana Naibu Katibu Mkuu awasiliane na wahariri wa habari wa vituo vya televisheni Channel 10, TBC1, Star TV, Mlimani TV na ITV ili niweze kutoa taarifa ya kuwasihi Waislam warudi majumbani na kwenye shughuli zao baada ya sala ya Ijumaa. Niliweza kufanya mahojiano na Channel 10, TBC1, na ITV. Kwa bahati mbaya Camera person wa Star TV alikuwa kwenye shughuli nyingine na kwa hiyo sikuweza kufanya mahojiano na Star TV. Vilevile wapiga picha wa Mlimani TV hawakuwepo kwenye studio. Pia nilipata bahati ya kuzungumza na Radio Iman inayosikilizwa na Waislam wengi na kueleza maoni yangu kuwa Waislam wasiandamane baada ya sala ya Ijumaa.
Baada ya kutoa taarifa kwenye vituo vitatu vya televisheni na Radio Iman kuwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wataachiliwa na kuwasihi Waislam wasishiriki maandamano baada ya sala ya Ijumaa nilimpigia simu Abdul Kambaya kuulizia kama naweza kuzungumza na Sheikh Ramadhan Sanze. Kambaya akanieleza mambo yamebadilika na hawajaachiwa. Niliwasiliana na RCO na nikabaini kuwa suala hilo haliko tena chini ya uamuzi wake na litakamilishwa siku ijayo.
Usiku wa alhamisi kuamkia Ijumaa nilijaribu kuwasiliana na Rais Kikwete kupitia wasaidizi wake ili nimfahamishe mantiki na sababu ya hatua nilizochukua na atumie uwezo wake alionao Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waachiliwe. Kwa bahati msaidizi mmoja alipata ujumbe wangu wa simu na akanipigia simu saa 6:50 usiku na kunifahamisha atajitahidi kuufikisha ujumbe wangu kwa Mhe. Rais ili nipate kuongea naye kuhusu jamaa wanaoshikiliwa na polisi waachiwe ili kupunguza jazba na kuepusha shari. Niliyezungumza naye alikuwa Dodoma na Rais alikuwa Arusha na ratiba yake ilikuwa imebana sana na kwa hiyo hakuweza kupata fursa ya kunipigia simu siku hiyo ya Ijumaa.
Siku ya Ijumaa Abdul Kambaya aliendelea kufuatilia kuachiwa kwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake Central Police Station. Nami katika kuhangaika ili waliokamatwa waachiliwe nilipata fursa ya kuzungumza na IGP na kumfahamisha sababu ya juhudi nilizochukua na mategemeo yangu kuwa Sheikh Sanze na wenzake wangeachiwa. Ninakiri kuwa katika mazungumzo ya simu, IGP Mwema alikuwa msikivu na mkarimu sana katika kauli yake. Alinishukuru kwa kauli niliyoitoa katika vituo vya televisheni na kuwa atafuatilia suala nililomueleza. Hatimaye Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waliachiwa.
Naamini kama Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wangeachiwa ingesaidia sana kupunguza jazba. Hata hivyo Waislam wengi na wananchi wengine kwa ujumla walipokea vizuri wito wangu na hawakushiriki katika maandamano. Baadhi wamenikosoa na kushauri kuwa ilifaa nisubiri mpaka baada ya maandamano kufanyika na kama patatokea majeruhi na vifo ndipo nitoe tamko la kulaani vitendo vya polisi na serikali.
Katika mitandao ya kijamii wengine wamekejeli juhudi zangu. Nilikubali kushiriki katika kipindi cha Makutano show kinachoendeshwa na Bi. Fina ambapo hupata maswali toka Jamii Forum. Moja ya swali lililotolewa ni “Muulize very very solid, kuna agenda gani kati ya Cuf na uislam? mtaani leo wanasema kauli ya Lipumba ya jana kusitisha maandamano wameitii, na ukiangalia mikutano yake pale jangwani utafikiri kuna mawaidha ni balaghashia na baibui.” Fina hakupata muda wa kuniuliza swali hili. Jibu lake ni la wazi. CUF inasimamia Haki Sawa kwa Wananchi Wote. Kuna Watanzania wengi ambao ni Waislam na wao pia wanastahiki kutendewa haki katika nchi yao. Kuhusu balaghashia na baibui ni vyema vijana wakatazama picha za umati wa watu uliokuwa unahutubiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa nchi hii. Picha hizo pia zinaonyesha waliokuwa wakipigania uhuru wengi walivaa balaghashia na baibui hata Mwalimu Nyerere alipewa zawadi nyingi za balaghashia na akaamua kuzivaa.
Kushamiri kwa demokrasia ya kweli msingi wake mkubwa ni amani na utulivu. Amani ya kweli haipatikani bila kuwepo haki. Kesi ya Sheikh Ponda msingi wake na madai ya kiwanja. Ki msingi kesi ya madai ya kusuluhishwa na Mahakama ya ardhi. Sheikh Ponda ana haki ya msingi ya kupewa dhamana hata kama kauli zake haziifurahishi serikali.
Nasikitika sana katika kipindi hiki tete, viongozi wa serikali wameshindwa kuchukua juhudi za makusudi kuzungumza na Maimam wa misikiti na viongozi wa asasi za Kiislam kupunguza jazba. Badala yake wameachia kauli za vitisho vya Kamanda Kova ndiyo viwe mawasiliano kati ya serikali na Waislam. Ni vyema serikali ikatumia busara na kuwasiliana na Maimamu wa misikiti na viongozi wa asasi za Kiislam kuelewa hoja na malalamiko yao.
Hatimaye nimepata fursa ya kuzungumza na Mheshimiwa Rais leo asubuhi na nikamueleza juhudi nilizozichukua kuweza kupunguza jazba na kuwaomba Waislam wasishiriki kwenye maandamano baada ya sala ya Ijumaa. Ni wazi hali hii ya mtafaruku ndani ya jamii inamsononesha sana Mheshimiwa Rais na ninaamini atajitahidi kwa uwezo wake wote kutafuta suluhisho.
Katika kutafuta suluhu ya mtafaruku huu nitaendelea na jitihada za kutafuta fursa niweze kubadilishana mawazo na Rais Kikwete. Nitazungumza na viongozi wa asasi za Kiislam. Nitazungumza na viongozi wa Makanisa ya Kikristo. Madhumuni ya mazungumzo yangu ni kuwafahamisha mantiki ya juhudi nilizofanya na kushauriana misingi muhimu ya Waumini wote kuheshimiana na kuvumiliana ili tujenge Tanzania yenye haki sawa kwa wote.

Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti
Novemba 4 2012