Mwenyekiti Wa Jumuiya ya Vijana Taifa-Mh Katani A Katani |
Mheshimiwa Mwenyekitiwa Chama Taifa,ProfIbrahim H. Lipumba
MheshimiwaMakamuMwenyekitiwa Chama Taifa, Mzee Hamisi Machano
Mheshimiwa Naibu katibu Mkuu Tanzania bara,
Waheshimi wa Wakurugenzi,
Waheshimi wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa,
Waheshimiwa Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama,Waheshimiwa Wanachama na Wananchi wote mliopo hapa,Waheshimiwa Vijana,
Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia sisi wote kukutana hapa kwa muda huu, pia nawashukuru nyinyi wote kwa kuwa nasi siku ya leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kwa niaba yaVijana wa Chama cha wananchi- CUF, na kwa niaba yaVijana wa Tanzania kupitia Secretariet yaVijanaTaifa na chukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kazi kubwa unayoifanya na nia safi unayoionyesha ya kutaka kuwakomboa Watanzania kutoka katika maisha duni na ya ukandamizwaji waliyonayo kwa sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tunapendaa utambue kuwa sisi Vijana wa Chama cha Wananchi-CUF na Watanzania kwa ujumla tunaamini uwezo wako katika suala zima la Uongozi waTaifa hili na ujenzi wa uchumi imara, utakaoleta maisha yenye tija kwa watanzania na kuwatoa katika janga la umasikini uliokithiri hasaVijana ambao,wengi wetu tumekuwa tukiishi katika maisha magumu na yasiyo na matumaini wala ndoto za mabadiliko kutokana na Mfumo mbovu wa Uongozi wa Serikali ya CCM.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tuna amini uwezo wako uliouonyesha tangu 1995 ulipoamua kutumia Elimu yako kwa maslahi ya watanzania bila kujali maslahi binafsi na famila yako, kwa kueleza Mipango na Dira ambayo ungepewa ridhaa ya kuongoza nchi hii ungeyatekeleza. Mengi uliyoyasema yanaonekana kutekelezeka,mfano Kodi ya manyanyaso imefutwa, ulisema Mtoto wa maskini asome bure limeetekelezwa ingawa lipo chini ya kiwango,upingaji wa ununuzi wa Rada na ndege ya Rais jambo ambalo leo limeonekana na kuleta madhara makubwa kwa watanzania, Sambamba na hayo ni wewe Mwenyekiti wetu ambaye uliyatolea tahadhari masuala ya IPTL, RICHMOND na DOWANS na kuyapigia kelele, ni wazi kuwa leo yamedhihiri na kuonekana ni Ufisadi mkubwa kwa Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tunakuhakikishia kuwa vijana wote wa Watanzania unaowaona hapa leo hii na waliobaki majumbani, wanandoto na matumaini makubwa na wanaamini hakuna Chama chochote wala kiongozi yeyote mwenye uwezo wa kuwaondolea matatizo yaliyodumu tangiakupatikana kwa Uhuru wa nchi hii 1961 hadi leo hii ambayo ni ukosefu wa Elimu bora, ukosefu wa ajira za kudumu na huduma mbovu zitolewazo za afya isipokuwa ni wewe ProfesaLipumba, hivyo wapo tayari kuhakikisha wanakupeleka Ikulu kupitia Chama hiki 2015.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kwa miaka 50 sasa Vijana wengi tumekuwa TUKITAABIKA NA KUATHIRIKA na MFUMO ULIOPO na kujikuta tukikosa haki zetu za msingi katika nchi hii, huku wachache wakinufaika na kuishi maisha ya Kidikteta kwa kutumia pato la Taifa linalotokana na rasilimali zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Ni kweli kuwa umekuwa mstari wa mbele kuelezea mapungufu ya Uongozi wa Serikali ya CCM na katika kulisimamia hili uliweza kufanya kongamano Diamond jubilee na kutoa kitabu kinachoelezea OMBWE LA UONGOZI kwa lengo la kuwa tahadharisha Watanzania juu yaUdhaifu na Uozo wa Serikali ya CCM, hali inayopelekea Nchi kuingia katika Migomo ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali.Lakusikitisha zaidi ni maandamano ya kila siku ya wanafunzi wa vyuo vikuu na sasa hivi imeanza kuenea elimu ya Msingi jambo ambalo linaonesha wazi kushindwa kwa serikaliya CCM.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Vijana wengi Watanzania, hasa sisi watoto wa makabwela tumekuwa tukibaguliwa katika kupata ELIMU BORA huku wenzetu watoto wa mabeapari na mafisadi wakubwa wa nchi hii wakipata ELIMU BORA tena ndani na nje ya nchi hii huku wakitumia kodi zinazotokana na pato la wazee wetu sote ambao wengi ni wakulima, Wafugaji, Wavuvi na wavujajasho wa nchi hii, jambo ambalo lina wafanya waendelee kututawala na kutukandamiza kiuchumi.
Mh Mwenyekiti,
Suala la ajira limekuwa donda ndugu kwetu vijana wengi tumekuwa tukiishi maisha magumu na ya kubahatisha kiasi cha kushindwa kujua kesho itakuwa vipi na hii inatokana na Mfumo uliopo wa Utawala na Mipango mibovu isiyo angalia matakwa na maslahiya wanannchi na hasa kuto kuwapa Vijana ELIMU BORA yakuwawezesha kujiajiri na kujiingizia kipatowenyewe.
Tunasema hali hii imetuchosha, haivumilikitena, hatuwezikuishi katika nchi hii kama watumwa hukuwenzetu wachache wakinufaika na kufaidi rasilimali za nchi pamoja na kutumia kodi za Wazee wetu.
Mh mwenyekiti,
Tunakuhakikishia Vijana wote tuliopo hapa tupot ayari kwa lolote na wakati wowote na kufanya chochote ili kuking’oa Chama cha Mapinduzi madarakani ifikapo 2015 na Mawakala wao waliojipa sura ya kupinga Ufisadi hali ya kuwa wao ndio vinara wakubwa wa Ufisadi nchini na wapo tayari kuiuza nchi kwa maslahi yao.
Tunatoa wito kwaVijana wote nchini kujiunga na jumuiyayaVijanawa Chama cha wananchi –CUF, na kugombea nafasi za Uongozi katika ngazi zote za Uongozi wa Chama na serikali kupitia jumuiya, kwa kuwa Jumuiya yaVijana-CUf ndio chombo pekee ambacho Vijana makabwela wanchihii wanaweza kupata fursa ya kupaza sauti juu ya matatizo yanayowakabili
Mh mwenyekiti,
Kaulimbiu yetuVijana ni
TOBOA GAMBA VUA GWANDA VAA HAKI JUINGE NA VISION FOR CHANGE (V4C) MCHAMCHAKA MPAKA 2015.
ImetayarishwaSekretarietiyaVijanaTaifa.
No comments:
Post a Comment