Thursday, September 6, 2012

MAUAJI YA RAIA NI MUHIMU MTAALA WA MAFUNZO YA POLISI KUANGALIWA UPYA


SEKRETARIETI ya Vijana Chama cha Wananchi –CUF (JUVCUF) Taifa tunataka Serikali kupitia upya MTAALA wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwapa elimu ya maadili mema katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu na jinsi ya kukabiliana na changamoto ndogondogo kama za Maandamano ya Raia na Mikutano ya hadhara inayofanyika kwa Sasa, hasa kutokana na kukua kwa Demokrasia hapa nchini .
Tunaamini bila ya Serikali kukaa na kuliangalia nini polisi wanatakiwa wafundishwe wanapokabiliana na raia wasiokuwa na silaha wala kujua matumizi yake, hali itazidi kuwa mbaya hapa nchini sababu Polisi wataendelea kukosa maadili, wataua na kujeruhi raia jambo litalowafanya raia nao kutembea na silaha za moto kila watapok...
uwa kwenye mikutano yao ya hadhara au Maandamano, na ikifikia hapo nchi itakuwa imepoteza amani yake iliyodumu kwa nusu karne sasa na itasababisha nchi kuingia kwenye machafuko kama ilivyotokea katika mataifa ya Afrika Kaskazini ambapo ilifika mahali vijana walichoshwa na vitendo vya mauji ya raia na kuamua kuasi wakapambana na Utawala hadi ukaanguka madarakani.

JUVCUF tunaamini kuwa Watanzania wengi hasa vijna wamekuwa wakiishi kwa utulivu huku wakilinda amani ya Taifa hili pamoja na matatizo makubwa ya umsikini yanowakabili kutokana na kukosekana kwa ajira za uhakika na kudumu kunakosababishwa na mfumo mbaya wa utawala na mipango hasi ya chama cha Mapinduzi.
Tunaiomba serikali kuwa makini na iwajengee uadilifu watendaji wake waliopo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kuheshimu Mkataba wa kimataifa wa haki za Binaadamu wa 1948 ili kulinda haki za msingi za binaadamu hapa nchini.
Vijana wa CUF tunaendelea kulaani mauji hayo yanayoendelea kufanywa na Polisi kwakuwa yamekiuka haki ya msingi ya kuishi ya Marehemu Mwangosi kijana ambae alikuwa bado anahitaji kulitumikia Taifa lake. Hivyo tunaomba Tume iliyoteuliwa iwe makini katika kuchunguza na kulifuatilia suala hili na iwe huru na yeyote aliyehusika atajwe na kufikishwa kwenye mikono ya sharia bila kujali nafas, umaarufu au uwezo wa kifedha alionao.
Tunawaomba Vijana wajiunge na kushirikiana na CUF ili tulete mabadiliko yenye tija na manufaa kwa Vijana yatayolinda haki ya kila kijana ndani ya nchi na kupambana na kuondoa uonevu kama huo unaofanywa na polisi kwa maslahi ya watu wachache.
Ashura Mustapha
Mkurugenzi Wa Habari Juvicuf

No comments:

Post a Comment