KAULI YA NAPE DHIDI YA CHADEMA NI KAMA MTU ANAEOGOPA KIVULI CHAKE
Mh Abdul Kambaya- Naibu Mkurugenzi wa Habari, Mahusiano na Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF)
CUF –Chama cha Wananchi kimeshangazwa na Kauli ya Katibu Muenezi wa
CCM, alietoa kwa Vyombo vya Habari na kukituhumu chama cha CHADEMA ,
kwamba kimeingia mikataba ya kufisadi na Wafadhili walionje ya Nchi kwa
lengo la kutaka kuja kupora Mali ya Asili inayoendelea kugunduliwa hapa
Nchini kwetu Tanzania. Katika maelezo yake Katibu huyo iliita kile
kilichofanywa na CHADEMA katika HARAMBEE ya kutafuta Fedha ni USANII, na
kwamba CHADEMA wanataka kuhalalisha mabilioni waliopata toka kwa
Wafadhili wao, na kwamba CCM inaushahidi na inawafahamu Wafadhili hao.
CUF –Chama cha Wananchi kinashangazwa na kauli hii ya kisanii
iliotolewa na CCM kupitia Katibu wake Muenezi, CCM ni Chama
kinachoongoza Nchi, jambo ambalo walipaswa kusema sio kuishitaki CHADEMA
kwa Wananchi bali ni kuzuia hayo babilioni na kuwataja hao wafadhili
ambao wameingia Mikataba na CHDEMA kwa lengo la kuja kupora utajiri
mkubwa unaoendelea kugunduliwa katika masiku ya hivi karibuni. CUF-
Chama cha Wananchi kinaamini kwamba CCM na CHADEMA ni watoto wa familia
moja , na Wanafadhili wanao wafadhili ni wa aina moja wa ndani na nje
ya Nchi. Iwapo Chadema wameingia mikataba ya kupewa mabilioni ili baadae
wataposhika Madaraka waweze kulipa mabilioni hayo kwa kutukmia Mali ya
asili tulionayo, basi watakuwa wanaendeleza utaratibu ule ule wa CCM wa
kuiuza Nchi kwa bei poa ili mradi wao wawepo madarakani kama ambavyo CCM
inafanya hivi sasa kuingia Mikatba mibovu isiokuwa na Manufa na
Wananchi ili mradi wao wawafurahishe Wafadhili wao. CUF- Chama cha
Wananchi kinaamini kwamba Mti wa Matatizo ya Nchi yetu, ni Mufumo
mbovu unaoendesha Serikali yetu na Nchi kwa ujumla wake. Kuwa na Vyama
vyenye tamaa ya Madaraka, kama CCM na Chadema, ni matokeo ya awali ya
Mfumo mbovu wa Nchi yetu, na kukithiri kwa wizi na matumizi mabaya ya
Fedha za Umma na ukiukwaji wa Haki za binaadamu ni matokeo ya kati ya
Mfumo mbovu. Watanzania waliowengi kuwa masikini wa kutupwa, ukosefu wa
huduma bora kwa jamii,kudumaa kwa maendeleo ya Nchi na ukosefu wa ajira
ni Matokeo ya muda mrefu yanayosababishwa na Mfumo mbovu wa Nchi yetu.
Kwa maana hiyo basi, CUF –Chama cha Wananchi kinaamini kwamba , njia
sahihi ya kulinda Rasilimali zilizopo na zinazoendelea kugunduliwa ndani
ya Nchi yetu, ni kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitafa, Serikali ambayo
itashirikisha Vyama vyote venye wabunge, na kwa utaratibu huo, kutakuwa
hakuna Chama kitakachokuwa na maauzi ya pekee katika matumizi ya
Rasilimali na Mali ya asili ya Nchi yetu. Jambo hili limekuwa
linahubiriwa sana na CUF , lakini pia limekuwa linapingwa sana na CCM
na Chadema na kwa mantiki hiyo, CUF – Chama cha Wananchi hakioni
tafauti ya CCM na Chadema kisera na kimtazamo. CUF kinawataka Watanzania
waelewe kwamba, kinachonekana hapa ni kwamba ,Chadema inaonyesha
imewazidi kete CCM huko kwa Wafadhili wa nje kama ilivyowazidi kete kwa
ufadhili wa Sabodo ndio maana unaona CCM inapiga kelele. CUF –
Chama cha Wananchi kina wataka CCM waache kuogopa kivuli chao na badala
yake washughulike na kubadili Mufumo unaoendesha Nchi yetu iwapo kweli
wanataka mabadiliko ya Kiuchumi na Kijamii .
No comments:
Post a Comment