Sunday, September 23, 2012

CHADEMA IMEDANDIA BEHEWA LA CUF!

Naibu katibu Mkuu JUVICF-Thomas Malima

Wengi tunaamini kuwa Elimu ni ufunguo wa maisha. Waandishi wamesomeshwa kwa kodi za watanzania kwa lengo la kupata elimu ya kuwahabarisha watanzania habari za ukweli na uhakika juu ya mustakabali wa maisha yao.

Lengo la elimu ni kujenga uwezo wa mambo makuu matatu kwa kila mwananchi ambayo ni uwezo wa kuhoji au kuuliza, uwezo wa kujifunza na uwezo wa kujiamini. Katika haya yote mkazo upo katika ubora na si vinginevyo, yaani kumjenga msomaji hasa mwandishi uwezo wa kufikiri, kusikiliza, kuuliza maswali, kupambanua na kuwasiliana na jamii bila kupotosha.

Baadhi ya waandishi wa habari nchini hawana uwezo uliotajwa hapo juu kutokana na kuandika makala zisizo na utafiti wala umakini kwa umma. Makala iliyoandikwa na mwandishi Mashaka Mgeta katika gazeti la Nipashe la tarehe 19 Septemba 2012 yenye kichwa CUF INAPOPANDIA BEHEWA LA CHADEMA ni ya kishabiki na yenye lengo la kuudanganya umma na zaidi ya yote imemdhalilisha mwandishi huyo pamoja na mhariri wa gazeti hilo kwa kuandika habari zisizo za utafiti.

CUF ilianza kauli mbiu yake ya VISION FOR CHANGE  mwaka 2008 na kuiweka rasmi kwenye Manifesto yake ya uchaguzi ya mwaka 2010. Tangu mwaka huo CUF haikuwahi kubadili kauli mbiu hiyo hadi wakati huu. Lakini cha kushangaza ni pale CHADEMA walipodandia kauli mbiu hiyo kwa kuzindua Movement for change M4C mwaka 2011. Ikumbukwe kuwa CUF iliinadi V4C nchi nzima wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 lakini leo baadhi ya waandishi wanajaribu  kuupotosha umma wa Watanzania kuwa CUF imedandia M4C ya CHADEMA. Je kwa ushahidi huo kati ya CUF na CDM nani amedandia hoja ya mwingine­­­­­?.

Hili si jambo la kwanza kwa CDM kuiga kutoka kwa CUF. Watanzania watakumbuka kuwa rangi za mwanzo za bendera ya CHADEMA  zilikuwa ni BLUE NA NYEUPE lakini baada ya kuona bendera za CUF zinavutia na zinaashiria mabadiliko ya kweli waliziiga na hatimaye kubadilisha bendera ya Chama chao ili zifanane na CUF kwa lengo la kuwatapeli wanachama na wafuasi wa CUF mikoani kuwa wao na CUF ni kitu kimoja hivyo wawape ushirikiano kwani wote ni wapinzani wa CCM.

CHADEMA pia waliendelea kuiga kauli  mbiu iliyokuwa inatumiwa na viongozi wa CUF kwenye mikutano yao. Watanzania watakumbuka kuwa  kaulimbiu ya mwanzo ya CHADEMA ilikuwa CHADEMA ……VEMA huku wakinyanyua vidole viwili. Lakini katika mkutano wa CUF kama chama kikuu cha upinzani kilichokuwa kinalea vyama vingine vidogo ikiwamo CHADEMA pale Viwanja vya BAKHRESSA mwaka 2004 ndipo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar mheshimiwa Juma Duni alipozindua kauli mbiu ya NGUVU YA UMMA….CHACHU YA MABADILIKO. Baada ya mkutano huo ulioshirikisha vyama vingine kama CHADEMA ndipo Viongozi wa CHADEMA walipoamua kubadilisha kauli mbiu yake kuwa PEOPLES …..POWER. Iweje leo watu wasahaulishwe ukweli wa nani si mbunifu na nani anayesubiria mwingine abuni ili yeye aje na kukopi?.

Watanzania watakumbuka kuwa tangu CUF ilipoanzishwa ilikuwa na hoja ya Tanzania kuwa serikali 3 wakati CHADEMA ilikuwa inadai serikali ya MAJIMBO. Lakini cha kushangaza leo hii CHADEMA wamehama katika hoja yao ya Serikali ya majimbo na kuanza kuibaka hoja ya CUF ya serikali 3. Je hili nalo hamulioni kuwa CHADEMA hawana jipya bali wanasubiri CUF waibue hoja na wao ndo wanaibukia juu kwa juu?.

Suala mahitaji ya Katiba Mpya nalo limeonesha kuwa CUF ndicho chama pekee kilicho kinara cha Mabadiliko nchini maana CUF imesimamia suala hilo tangu kuasisiwa kwake hadi leo. WanaCUF walifikia hatua ya kufyatuliwa Risasi za Moto na kuwaangamiza zaidi ya wanaCUF 40 nchi nzima. Lakini leo juhudi hizo zinaelekea kupotezwa. Ni CUF pekee ndiyo ilikuwa na agenda ya Katiba mpya tangu 1995 lakini CDM imekuja kujitokeza 2010 tu. Je hapa pia hawakudandia hoja ya CUF ya Katiba mpya?.

Watanzania watakumbuka kuwa Mwenyekiti wa CUF alipotoka Marekani mwanzoni mwa mwaka huu aliwaeleza watanzania namna ambavyo rasilimali za nchi hii zikitumika vizuri zinaweza kuleta mabadiliko na kuwanufaisha watanzania. Profesa Lipumba alisema hayo baada ya kufanya utafiti kwa muda wa miezi 6 nchini Marekani , ambapo alipendekeza kuwaomba wapenzi na wanachama wa vyama vya siasa kuchangia vyama vyao ili vipate nguvu ya kifedha itakayoleta mabadiliko kwa kuingoa CCM. Baada ya kutoa hotuba hiyo,CHADEMA waliamua kufanya harambee ya kuchangia chama chao mwanzoni mwa mwezi juni 2012. Cha ajabu CUF waliofanyia utafiti uchangiaji huo, walipoamua kuweka katika vitendo juzi, wanaCHADEMA wameibuka na kusema CUF imewaiga. Je, kati ya CUF iliyotumia miezi 6 kutafiti na CHADEMA walioiga baada utafiti wa CUF nani amedandia hoja ya mwingine?.

Mwisho napenda kutoa wito kwa watanzania kutambua kuwa kila wanachokiona kinafanywa na CUF leo kimefanyiwa utafiti wa kina na kuthibitika kuwa kinafaa. CUF itaendelea kuwa baba wa ubunifu kwa vyama vyingine. CHADEMA wataendelea kuiga kutoka kwa CUF maana viongozi wake bado ni wababaishaji na wapiga domo tu.


Thomas D.C Malima
                         
  Mwandishi wa makala hii ni Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya vijana ya CUF-Chama cha Wananchi na anapatikana kwa simu namba 0715172256 na e-mail thommalima@yahoo.com.



Sunday, September 16, 2012

TANZANIA TUKO NYUMA SANA KATIKA USHINDANI WA KIUCHUMI WA KIMATAIFA

Mwenyekiti Cuf Taifa- Prof Ibrahim Lipumba

Taarifa ya kila mwaka inayotolewa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya World Economic Forum (WEF) kuhusu ushindani wa kiuchumi wa mataifa(The Global Competitiveness Report 2012/13) inaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 120 kati ya nchi 144 wakati nchi jirani ya Rwanda imeshika nafasi ya 63.
Nchi inayoongoza kwa ushindani wa kiuchumi wa mataifa ni Uswissi (Switzerland), ikifuatiwa na Singapore, Finland, Uswidi (Sweden), Uholanzi (Netherlands), Ujerumani, Marekani, Uingereza, Hongkong na Japan.
Katika nchi za Afrika inayoongoza kwa ushindani wa kiuchumi ni Afrika ya Kusini inayoshika namba ya 52, ikifuatiwa na Mauritius ambayo ni ya 54 na ya tatu ni Rwanda iliyoshika nafasi ya 63 katika orodha ya nchi 144.
Watafiti wa WEF wanaeleza kuwa ushindani wa uchumi wa taifa unatokana na asasi za uchumi na utawala, sera, raslimali na nguvukazi (raslimali watu) zinazobainisha kiwango cha tija katika uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi na kwa hiyo kuiwezesha nchi kukuza uchumi kwa kasi, kuongeza utajiri wa nchi na neema kwa wananchi wake.
Ili kupima ushindani wa kiuchumi wa kila nchi, watafiti wamechunguza mambo ya msingi yanayochochea ukuaji wa uchumi na uletaji wa maendeleo kwa ujumla. Nchi zenye ushindani wa kiuchumi zinafanikiwa kuongeza ufanisi na tija katika uzalishaji wa bidhaa na usambazaji wa huduma. Zinatumia vizuri raslimali na nguvukazi na kwa hiyo kufanikiwa kukuza uchumi kwa muda mrefu. Katika ulimwengu wa utandawazi ambapo nchi zina fursa ya kuuza na kununua bidhaa na huduma katika soko la dunia ushindani wa kiuchumi ni nyenzo muhimu ya kuongeza kasi ya kukuza uchumi kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Watafiti wa WEF wanaanda kielelezo (farihisi) cha ushindani wa uchumi wa mataifa. Kielelezo hiki kutunamia vigezo vingi kupima ushindani wa kiuchumi unaotokana na asasi, sera, raslimali na vipengele vingine ambavyo vinabainisha uwezo, ufanisi na kiwango cha tija katika uzalishaji mali wa sekta mbali mbali za uchumi na huduma. Kiwango cha tija na ufanisi katika uzalishaji ndicho kinachovutia uwekezaji wa ndani na nje na kuchochochea ukuaji wa uchumi na ongezeko la wastani la pato la kila mwananchi.
Utafiti wa WEF umebaini nguzo 12 za ushindani wa kiuchumi wa mataifa. Nguzo ya kwanza ni asasi za uchumi, utawala na sheria ambazo zinajenga mazingira ya kushirikiana katika shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja, kampuni na serikali katika shughuli za uzalishaji na kuongeza utajiri wa taifa. Umuhimu wa mfumo wa asasi ulio wazi na kufanya kazi kwa ufanisi na haki umebainika hata kwa nchi zilizoendelea baada ya mtikisiko na mgogoro wa sekta ya fedha ulioanza Marekani mwaka 2008 na kuikumba dunia yote. Ukosefu na udhaifu wa usimamizi wa asasi za fedha katika nchi zilizoendelea na hasa Marekani ndiyo chanzo cha kuporomoka na kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa muda wa miaka minne iliyopita.
Ubora wa asasi za uchumi na utawala ni jambo la msingi katika ushindani wa kiuchumi wa kila taifa. Mfumo na utendaji wa asasi hizi ndiyo unaoshawishi uwekezaji wa vitega uchumi na uzalishaji wa bidhaa na huduma. Mfumo wa asasi ndiyo kigezo muhimu cha mgawanyo wa pato la taifa na gharama za utekeleza wa mikakati ya kukuza uchumi. Kwa mfano kuwepo kwa hakimiliki za kuaminika ni muhimu sana katika kushawishi uwekezaji. Ikiwa mali ya mtu inaweza kuporwa kwaurahisi na watu wengine au serikali, uwekezaji wa vitega uchumi utapungua.
Ubora wa mfumo wa asasi ni pamoja na kuwepo utawala bora, ufanisi katika shughuli na usambazaji wa huduma za serikali, kutokuwepo kwa rushwa, ukusanyaji mzuri wa kodi na uadilifu katika matumizi ya fedha za umma. Utendaji, ufanisi na maadili ya sekta binafsi yanachangia katika kujenga ushindani wa kiuchumi wa taifa husika.
Nguzo ya pili ya ushindani wa kiuchumi ni miundombinu. Miundombinu inayojumlisha usafiri- barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege; ufuaji na usambazaji wa umeme; ugawaji na usambazaji wa maji; miundombinu ya majitaka, na miundombinu ya mawasiliano inayoharikisha upeanaji wa taarifa na habari. Ubora wa miundombinu unachangia sana katika kuongeza ufanisi na tija ili kukuza uzalishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Nguzo ya tatu ni utengamavu wa uchumi mpana (macroeconomic stability) kwa maana ya mfumko wa bei wa kadri, riba ziwe za nafuu na pasiwe na tofauti kubwa sana kati ya riba ya mikopo na riba wanaolipwa waweka akiba,  thamani ya sarafu iwe tengamavu na ya ushindani kwa wazalishaji wa bidhaa na huduma wa ndani ya nchi, akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ya kuagizia bidhaa na huduma za nje, matumizi ya serikali yasizidi mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa. Utengamavu wa uchumi mpana pekee haukuzi uchumi, bali unajenga mazingira ya kuvutia uwekezaji na ukuaji wa uchumi ikiwa mambo mengine kama vile miundombinu na asasi bora vipo. Kutokuwepo kwa utengamavu wa uchumi mpana kunaathiri motisha wa uwekezaji na uzalishaji kwani kunaweka mashaka makubwa kwa bei halisi za raslimali, nguvukazi, bidhaa na huduma mbalimbali.
Nguzo ya nne ni afya na elimu bora ya msingi. Wananchi wenye afya njema wana uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na tija ya juu. Wananchi weye afya mbovu siyo wazalishaji wazuri. Afya duni inaongeza gharama za uzalishaji. Ubora wa elimu ya msingi kwa wananchi wote inawezesha wafanyakazi waweze kufundishika. Wafanyakazi wasiokuwa na elimu bora ya msingi na kujua kusoma vizuri siyo wepesi kujifunza teknolojia mpya ya uzalishaji.
Nguzo ya tano ni elimu na mafunzo ya juu. Elimu bora ya juu na hususan elimu ya sayansi na teknolojia ni muhimu kwa nchi zinazohitaji kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na bidhaa za teknolojia. Katika ulimwengu wa utandawazi , kuwa na watu wenye elimu ya juu ya sayansi na teknolojia ni muhimu katika kujenga ushindani wa uzalishaji wa bidhaa za kisasa.
Nguzo ya sita ni ufanisi wa soko la bidhaa. Nchi zenye masoko ya bidha yenye ufanisi na ushindani halali yanavutia uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma bora. Ushindani wa soko ni muhimu katika kumotisha uvumbuzi na ufanisi katika uzalishaji. Kodi za juu zinaondoa motisha na kuathiri ushindani wa kiuchumi. Katika soko ambalo wateja wake wana utamaduni wa kutaka bidhaa bora unasaidia kulazimisha kampuni zishindane katika kuzalisha bidhaa bora.
Nguzo ya saba ni ufanisi wa soko la ajira. Ufanisi na mnyumbuliko wa soko la ajira ni jambo la msingi katika kuhakikisha kuwa watu wanaajiriwa katika nyanja ambazo watakuwa na uzalishaji wenye tija kubwa kulingana na uwezo na ujuzi wao. Uchumi unaokua kwa kasi kubwa na kubadilika mfumo wake unahitaji wafanyakazi wapungue kwenye sekta zinazodidimia au kutoweka kabisa na waongezeke  katika sekta zinazokua kwa kasi. Bila kuwepo kwa mnyumbuliko wa soko la ajira, mabadiliko ya haraka ya mfumo wa uchumi kama vile kupungua kwa sekta ya kilimo na kuongezeka kwa sekta ya viwanda, hayawezi kutokea. Soko la ajira lenye ufanisi linawapa mishahara mizuri wafanyakazi hodari na makini ili kuwapa motisha wa kuendelea kuchapa kazi. Wafanyakazi wavivu na wazembe wanapata kipato kidogo ukilinganisha na wafanyakazi hodari. Wafanyakazi wote wanajua kuwa wakiendelea na uzembe watapoteza ajira.
Nguzo ya nane ni maendeleo ya soko la mitaji na huduma za fedha. Uchumi wa kisasa unahitaji huduma za mikopo na mitaji. Ukusanyaji wa akiba kwa ufanisi unaruhusu kuwepo kwa mikopo yenye riba nafuu. Akiba itumiwe vizuri kuwapa mikopo wazalishaji wenye tija ya juu. Benki na taasisi nyingine za fedha zina kazi ya kutambua wajasiriamali wenye miradi mizuri yenye tija na kuwakopesha mitaji. Kuwepo kwa benki na taasisi nyingine za fedha zinazofanya kazi kwa ufanisi kunachochea ukuaji wa uchumi.
Nguzo ya tisa ni utayari wa kiteknolojia. Katika ulimwengu wa utandawazi ambapo kuna mabadiliko ya mara kwa mara ya teknolojia ni muhimu kwa nchi kujenga uwezo wa wananchi na kampuni zilizomo nchini kupokea, kumudu na kutumia teknolojia mpya. Hivi sasa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) imekuwa na matumizi katika nyanja zote za uzalishaji, elimu, afya na huduma nyingine. Taifa lenye miundombinu ya TEHAMA na wafanyakazi na jamii inayoweza kutumia TEHAMA ina fursa ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa ufanisi wa juu, kuongeza tija na kukuza uchumi.
Nguzo ya kumi ni ukubwa wa soko. Ukubwa wa soko unatoa fursa kwa uzalishaji mkubwa unaopunguza wastani wa gharama za uzalishaji. Nchi zenye soko kubwa la ndani inaweza kuanzisha na kuimarisha kampuni za uzalishaji kwa kutegemea soko la ndani. Katika ulimwengu wa utandawazi, soko la dunia linatoa fursa kwa nchi ndogo, kupunguza wastani wa gharama za uzalishaji kwa kuuza bidhaa na huduma zake kwenye soko la nje ya nchi. Kwa nchi ndogo kushiriki katika soko la dunia hasa kwa kuuza bidhaa za viwandani kunaongeza kasi ya kukua kwa uchumi.
Nguzo ya 11 ni kuwepo kwa kampuni na ufanyaji biashara wa kisasa. Kampuni ndio vituo vya uzalishaji vinavyotumia teknolojia mpya kuongeza ufanisi na tija. Ubora wa mtandao wa biashara na kuwepo kwa kampuni za kisasa zenye mikakati na uendeshaji wenye ufanisi kunaongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi. Nguzo hii ni muhimu zaidi kwa nchi zilizo mstari wa mbele katika maendeleo ya uchumi. Klasta (kishada) za kampuni za kisasa katika eneo moja zinasaidia sana katika uvumbuzi wa teknolojia mpya za uzalishaji wa bidhaa na usambazaji wa huduma. Klasta ya bonde la silicon (Silicon Valley), California, Marekani limechangia katika uvumbuzi mbalimbali wa TEHAMA.
Nguzo ya 12 ni uwezo wa uvumbuzi wa teknolojia mpya za uzalishaji wa bidhaa na usambazaji wa huduma. Uvumbuzi wa teknolojia mpya ndiyo unaochochea ukuaji na maendeleo ya uchumi kwa nchi zilizoko mstari wa mbele wa maendeleo kama vile Marekani, Ujerumani, Japan, Uswidi (Sweden) Uingereza, Uswissi (Switzerland) na zinginezo.
Nguzo hizi 12 za ushindani wa kiuchumi wa kimataifa zinahusiana. Nchi ikiwa dhaifu katika eneo moja basi kutakuwa na uwezekano wa kuwa dhaifu katika maeneo mengine. Kwa mfano uwezo wa uvumbuzi wa teknolojia hauwezi kuwepo bila kuwa na raslimali watu yenye afya njema na elimu nzuri na yenye uwezo wa kumudu teknolojia. Mfumo mzuri wa benki na soko la mitaji unahitajika ili kuhakikisha uvumbuzi wa teknolojia mpya yenye tija unafikishwa sokoni na kutumiwa katika uzalishaji wa bidhaa na usambazaji wa huduma.
Umuhimu wa nguzo moja moja kati ya nguzo zote 12 katika kuongeza ushindani wa kiuchumi wa mataifa na kwa hiyo kuchochea ukuaji wa uchumi unategemea hatua ya maendeleo iliyofikiwa na nchi husika. Njia bora ya Tanzania kuongeza ushindani wake wa kiuchumi siyo sawa na Uswidi kwani Tanzania ni maskini ina miundombinu mibovu na Uswidi iko mstari wa mbele katika maendeleo ya kiuchumi na teknolojia. Mishahara ya Uswidi ni ya juu wakati mishahara ya Tanzania ni ya chini na wananchi wachache sana wenye ajira za uhakika. Watanzania wengi wanategemea kilimo cha kujikimu na sekta isiyo rasmi.
Ukuaji wa uchumi katika nchi ambazo ziko chini kimaendeleo kama vile Tanzania kunategemea utumiaji wa ardhi na maliasili nyingine, na nguvukazi isiyokuwa na elimu na mafunzo ya kutosha. Kampuni zake zinashindana zaidi kwa bei za bidhaa za kawaida. Katika nchi zilizo katika hatua ya mwanzo ya maendeleo, ushindani wa kiuchumi unategemea nguzo ya kwanza ya asasi za uchumi, utawala na sheria, nguzo ya pili ya miundombinu, nguzo ya tatu ya utengamavu wa uchumi mpana (macroeconomic stability) na nguzo ya nne ya afya na elimu bora ya msingi.
Kwa kadri nchi inavyoendelea na kukamilisha matakwa ya nguzo ya kwanza mpaka ya nne ndivyo mishahara inavyoongezeka , ukuaji wa uchumi utategemea sana ongezeko la ufanisi katika uzalishaji na kuongeza ubora wa bidhaa. Katika hatua hii ya maendeleo iliyofikiwa na nchi kama Mauritius, Namibia na Afrika ya Kusini, ongezeko la tija na ukuaji wa uchumi unategemea nguzo ya tano ya elimu na mafunzo ya juu, nguzo ya sita ya ufanisi wa soko la bidhaa, nguzo ya saba ya ufanisi wa soko la ajira, nguzo ya nane ya maendeleo ya soko la mitaji na huduma za fedha, nguzo ya tisa ya utayari wa kiteknolojia, na  nguzo ya kumi ya ukubwa wa soko la ndani na uwezo wa kushindana katika soko la nje
Nchi zilizo mstari wa mbele katika maendeleo zinategemea zaidi nguzo ya 11 ya kuwepo kwa kampuni bora na ufanyaji biashara wa kisasa na nguzo ya 12 ya  uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kuongeza ushindani wa kiuchumi. Lakini nguzo nyingine pia ni muhimu. Kwa mfano miundombinu ya Marekani ikiwa ni pamoja na barabara na reli zinahitaji ukarabati mkubwa. Vilevile ubora wa elimu ya msingi na sekondari wa Marekani hasa katika shule za serikali katika maeneo ya watu masikini umeporomoka sana na unahitaji sera mwafaka ili ubora wa shule hizi ukaribie shule za nchi nyingine zilizoendelea.
Katika Taarifa ya WEF ya mwaka 2012/13, Rwanda imepanda nafasi 7  na kuwa ya 63 ukilinganisha na Taarifa ya mwaka 2011/12 ambapo ilikuwa ya 70. Rwanda inasifika kwa kuwa na asasi imara zinazozuia rushwa. Soko la ajira lina ufanisi na mnyumbuliko wa kutosha. Mabenki na soko la mitaji yameimarika na yanafanya kazi nzuri ya kukusanya akiba na kuwekeza vitega uchumi. Rwanda imewekeza kwenye TEHAMA na kuongeza kwa kiasi kikubwa utayari wake wa kiteknolojia. Kwa kuwa Rwanda haina bandari, ushindani wake wa kiuchumi unakwazwa na miundombinu ya nchi jirani ambako inalazimika kupitisha bidhaa zake.
Tanzania ilikuwa ya 120 katika Taarifa ya WEF ya mwaka 2011/12 na bado imebakia katika nafasi hiyo katika Ripoti ya 2012/13. Tanzania iko chini sana katika ushindani wa kiuchumi kwa sababu ya miundombinu mibovu. Tanzania ni ya 132 kati ya nchi 144 kwa ubora wa miundombinu. Tanzania bado iko chini katika elimu ya sekondari na elimu ya juu. Inashikilia nafasi ya 137 kati ya nchi 144. Tanzania pia iko chini sana katika utayari wa kupokea, kumudu na kutumia teknolojia na hasa matumizi ya mtandao wa internet ambapo inashikilia nafasi ya 122.
Ili Tanzania iweze kushindana na kunufaika katika ulimwengu wa utandawazi inahitaji iwekeze katika miundombinu ya barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege, ufuaji na usambazaji wa umeme, miundombinu ya maji safi na maji taka TEHAMA na kuboresha elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu. Ikiwa Rwanda imeweza kuongeza ushindani wake wa kiuchumi hakuna sababu kwa nini Tanzania ishindwe kufanya hivyo. Nchi inahitaji uongozi wenye dira, uadilifu na matumizi mazuri ya fedha za umma kuimarisha miundombinu na kuwekeza kwenye elimu bora ya vijana. Bila kuimarisha ushindani wa kiuchumi hatuwezi kuongeza ajira katika sekta za uchumi za kisasa.

Monday, September 10, 2012

HESHIMA KWENYE WIMBO WA CHAMA

UMATI WA WANACUF JANGWANIE

UMATI WA WANACUF JANGWANIE

UMATI ULIOFULIKA JANGWANI

UMATI WA WANACUF JANGWANI

KADI ZA MAGAMBA NA MAGWANDA ZILIRUDISHWA



Hizi ni baadi ya Kadi za ccm na chadema zilizo rusdiswa kwenye mkutano wa tarehe 09/09/2012 uliofanyika viwanja vya jagwani, mpata tunairusha habari hii kadi za ccm zilizorudishwa zilikuwa 319 na za chadema zilikuwa 201, katika hizo za chadema moja ni ya aliyekuwa KATIBU MUENEZI WA CHADEMA WA WILAYA YA WETE Ndugu ALLY ISSA MOHAMED OMARY

RISALA YA VIJANA WA CHAMA CHA WANANCHI- CUF MKUTANO WA JANGWANI 09/09/2012

Mwenyekiti Wa Jumuiya ya Vijana Taifa-Mh Katani A Katani
Mheshimiwa Mwenyekitiwa Chama Taifa,ProfIbrahim H. Lipumba
MheshimiwaMakamuMwenyekitiwa Chama Taifa, Mzee Hamisi Machano
Mheshimiwa Naibu katibu Mkuu Tanzania bara,
Waheshimi wa Wakurugenzi,
Waheshimi wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa,
Waheshimiwa Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama,Waheshimiwa Wanachama na Wananchi wote mliopo hapa,Waheshimiwa Vijana,

Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia sisi wote kukutana hapa kwa muda huu, pia nawashukuru nyinyi wote kwa kuwa nasi siku ya leo.


Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kwa niaba yaVijana wa Chama cha wananchi- CUF, na kwa niaba yaVijana wa Tanzania kupitia Secretariet yaVijanaTaifa na chukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kazi kubwa unayoifanya na nia safi unayoionyesha ya kutaka kuwakomboa Watanzania kutoka katika maisha duni na ya ukandamizwaji waliyonayo kwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tunapendaa utambue kuwa sisi Vijana wa Chama cha Wananchi-CUF  na Watanzania kwa ujumla tunaamini uwezo wako katika suala zima la Uongozi waTaifa hili na ujenzi wa uchumi imara, utakaoleta maisha yenye tija kwa watanzania na kuwatoa katika janga la umasikini uliokithiri hasaVijana ambao,wengi wetu tumekuwa tukiishi katika maisha magumu na yasiyo na matumaini wala ndoto za mabadiliko kutokana na Mfumo mbovu wa Uongozi wa Serikali ya CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tuna amini uwezo wako uliouonyesha tangu 1995 ulipoamua kutumia Elimu yako kwa maslahi ya watanzania bila kujali maslahi binafsi na famila yako, kwa kueleza Mipango na Dira ambayo ungepewa ridhaa ya kuongoza nchi hii ungeyatekeleza. Mengi uliyoyasema yanaonekana kutekelezeka,mfano Kodi ya manyanyaso imefutwa,  ulisema Mtoto wa maskini asome bure limeetekelezwa ingawa lipo chini ya kiwango,upingaji wa ununuzi wa Rada na ndege ya Rais jambo ambalo leo limeonekana na kuleta madhara makubwa kwa watanzania, Sambamba na hayo ni wewe Mwenyekiti wetu ambaye uliyatolea tahadhari masuala ya IPTL, RICHMOND na DOWANS na kuyapigia kelele, ni wazi kuwa leo yamedhihiri na kuonekana ni Ufisadi mkubwa kwa Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Tunakuhakikishia kuwa vijana wote wa Watanzania unaowaona hapa leo hii na waliobaki majumbani, wanandoto na matumaini makubwa na wanaamini hakuna Chama chochote wala kiongozi yeyote mwenye uwezo wa kuwaondolea matatizo yaliyodumu tangiakupatikana kwa Uhuru wa nchi hii 1961 hadi leo hii ambayo ni ukosefu wa Elimu bora, ukosefu wa ajira za kudumu  na huduma mbovu zitolewazo za afya isipokuwa ni wewe ProfesaLipumba, hivyo wapo tayari kuhakikisha wanakupeleka Ikulu kupitia Chama hiki 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kwa miaka 50 sasa Vijana wengi tumekuwa TUKITAABIKA NA KUATHIRIKA na MFUMO ULIOPO na kujikuta tukikosa haki zetu za msingi katika nchi hii, huku wachache wakinufaika na kuishi maisha ya Kidikteta kwa kutumia pato la Taifa linalotokana na rasilimali zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Ni kweli kuwa umekuwa mstari wa mbele kuelezea mapungufu ya Uongozi wa Serikali ya CCM na katika kulisimamia hili uliweza kufanya kongamano Diamond jubilee na kutoa kitabu kinachoelezea OMBWE LA UONGOZI kwa lengo la kuwa tahadharisha Watanzania juu yaUdhaifu na Uozo wa Serikali ya CCM, hali inayopelekea Nchi kuingia katika Migomo ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali.Lakusikitisha zaidi ni maandamano ya kila siku ya wanafunzi wa vyuo vikuu na sasa hivi imeanza kuenea elimu ya Msingi jambo ambalo linaonesha wazi kushindwa kwa serikaliya CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti,
Vijana wengi Watanzania, hasa sisi watoto wa makabwela tumekuwa tukibaguliwa katika kupata ELIMU BORA huku wenzetu watoto wa mabeapari na mafisadi wakubwa wa nchi hii wakipata ELIMU BORA tena ndani na nje ya nchi hii huku wakitumia kodi zinazotokana na pato la wazee wetu sote ambao wengi ni wakulima, Wafugaji, Wavuvi na wavujajasho wa nchi hii, jambo ambalo lina wafanya waendelee kututawala na kutukandamiza kiuchumi.

Mh Mwenyekiti,
Suala la ajira limekuwa donda ndugu kwetu vijana wengi tumekuwa tukiishi maisha magumu na ya kubahatisha kiasi cha kushindwa kujua kesho itakuwa vipi na hii inatokana na Mfumo uliopo wa Utawala na Mipango mibovu isiyo angalia matakwa na maslahiya wanannchi na hasa kuto kuwapa Vijana  ELIMU BORA yakuwawezesha kujiajiri na kujiingizia kipatowenyewe.

Tunasema hali hii imetuchosha, haivumilikitena, hatuwezikuishi katika nchi hii kama watumwa hukuwenzetu wachache wakinufaika na kufaidi rasilimali za nchi pamoja na kutumia kodi za Wazee wetu.

Mh mwenyekiti,
Tunakuhakikishia Vijana wote tuliopo hapa tupot ayari kwa lolote na wakati wowote na kufanya chochote ili kuking’oa Chama cha Mapinduzi madarakani ifikapo 2015 na Mawakala wao waliojipa sura ya kupinga Ufisadi hali ya kuwa wao ndio vinara wakubwa wa Ufisadi nchini na wapo tayari kuiuza nchi kwa maslahi yao.

Tunatoa wito kwaVijana wote nchini kujiunga na jumuiyayaVijanawa Chama cha wananchi –CUF, na kugombea nafasi za Uongozi katika ngazi zote za Uongozi wa Chama na serikali kupitia jumuiya, kwa kuwa Jumuiya yaVijana-CUf ndio chombo pekee ambacho Vijana makabwela wanchihii wanaweza kupata fursa ya kupaza sauti juu ya matatizo yanayowakabili


Mh mwenyekiti,
Kaulimbiu yetuVijana ni
TOBOA GAMBA VUA GWANDA VAA HAKI JUINGE NA VISION FOR CHANGE (V4C) MCHAMCHAKA MPAKA 2015.

ImetayarishwaSekretarietiyaVijanaTaifa.


Thursday, September 6, 2012

MAUAJI YA RAIA NI MUHIMU MTAALA WA MAFUNZO YA POLISI KUANGALIWA UPYA


SEKRETARIETI ya Vijana Chama cha Wananchi –CUF (JUVCUF) Taifa tunataka Serikali kupitia upya MTAALA wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwapa elimu ya maadili mema katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu na jinsi ya kukabiliana na changamoto ndogondogo kama za Maandamano ya Raia na Mikutano ya hadhara inayofanyika kwa Sasa, hasa kutokana na kukua kwa Demokrasia hapa nchini .
Tunaamini bila ya Serikali kukaa na kuliangalia nini polisi wanatakiwa wafundishwe wanapokabiliana na raia wasiokuwa na silaha wala kujua matumizi yake, hali itazidi kuwa mbaya hapa nchini sababu Polisi wataendelea kukosa maadili, wataua na kujeruhi raia jambo litalowafanya raia nao kutembea na silaha za moto kila watapok...
uwa kwenye mikutano yao ya hadhara au Maandamano, na ikifikia hapo nchi itakuwa imepoteza amani yake iliyodumu kwa nusu karne sasa na itasababisha nchi kuingia kwenye machafuko kama ilivyotokea katika mataifa ya Afrika Kaskazini ambapo ilifika mahali vijana walichoshwa na vitendo vya mauji ya raia na kuamua kuasi wakapambana na Utawala hadi ukaanguka madarakani.

JUVCUF tunaamini kuwa Watanzania wengi hasa vijna wamekuwa wakiishi kwa utulivu huku wakilinda amani ya Taifa hili pamoja na matatizo makubwa ya umsikini yanowakabili kutokana na kukosekana kwa ajira za uhakika na kudumu kunakosababishwa na mfumo mbaya wa utawala na mipango hasi ya chama cha Mapinduzi.
Tunaiomba serikali kuwa makini na iwajengee uadilifu watendaji wake waliopo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kuheshimu Mkataba wa kimataifa wa haki za Binaadamu wa 1948 ili kulinda haki za msingi za binaadamu hapa nchini.
Vijana wa CUF tunaendelea kulaani mauji hayo yanayoendelea kufanywa na Polisi kwakuwa yamekiuka haki ya msingi ya kuishi ya Marehemu Mwangosi kijana ambae alikuwa bado anahitaji kulitumikia Taifa lake. Hivyo tunaomba Tume iliyoteuliwa iwe makini katika kuchunguza na kulifuatilia suala hili na iwe huru na yeyote aliyehusika atajwe na kufikishwa kwenye mikono ya sharia bila kujali nafas, umaarufu au uwezo wa kifedha alionao.
Tunawaomba Vijana wajiunge na kushirikiana na CUF ili tulete mabadiliko yenye tija na manufaa kwa Vijana yatayolinda haki ya kila kijana ndani ya nchi na kupambana na kuondoa uonevu kama huo unaofanywa na polisi kwa maslahi ya watu wachache.
Ashura Mustapha
Mkurugenzi Wa Habari Juvicuf

Tuesday, September 4, 2012

CUF TUNALAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA CHANNEL TEN – IRINGA



Mwenyekiti Wa Cuf Taifa Prof Ibrahim Lipumba-Wa Pili Kushoto akisoma
Tamko,kulia kwake ni Mh Kambaya, kushoto kwake ni Mh Mketo na Mh
Chalamila.
CUF – Chama cha Wananchi tunalaani mauaji ya mwandishi wa Habari wa Channel Ten kituo cha Mkoa wa Iringa yaliyofanywa na jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo (IPC) Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kupigwa na bomu (kama inavyosemekana) katika vurugu za kisiasa baina ya Jeshi la Polisi na Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juzi Jumapili, Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa taarifa zinazotatanisha zilizotolewa na Vyombo vya Habari pamoja na kunukuu taarifa za jeshi la Polisi, kuwa Mwandishi huyo aliuwawa kwa mlipuko akiwa mikononi mwa jeshi hilo la Polisi hadi kupelekea hata Askari Polisi waliokuwa karibu yake kujeruhiwa na mwengine kukimbizwa Hospitali.
Taarifa hizo zinazotatanisha zinasema kwamba Mwandishi huyo alikimbilia kwa jeshi la Polisi kama kujisalimisha hadi kufikia kukumbatiana na OCS aliyekuwepo katika eneo hilo la tukio hili ni kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, lakini wakati huohuo vyombo hivyo hivyo vya Habari  vinaripoti kuwa Marehemu alikwenda kumtetea mwandishi mwenzake wa vyombo vya IPP Media na Polisi huyo OCS alikuwa akimuhami marehemu asiendelee kupata kipigo kutoka kwa askari wenzake kwani alikuwa akimfahamu, ndipo hapo alipopigwa na mlipuko huo na kutawanya matumbo yake nje.
Tukio kama hili la mauaji  kwa raia katika vurugu za kisiasa baina ya wafuasi wa CHADEMA na Jeshi la Polisi si la kwanza, ukiacha lile lililotokea siku za nyuma kule Arusha lililopelekea watu watatu kuuawa, tukio jengine la kusikitisha ni lile lililotokea Agosti 27, Jumatatu ya wiki iliyopita mjini Morogoro ambapo mtu mmoja alietambulika kwa jina la Ali Nzona (Muuza magazeti) alieuwawa katika vurugu kama hizo, ambapo taarifa zake zinautata wakati ambapo CHADEMA wakidai ameuwawa kwa risasi, taarifa ya Jeshi la Polisi inasema ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.
Inasemekana kuwa chanzo cha vurugu zote hizi za Morogoro na Iringa, ni kwa sababu Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekaidi amri ya Jeshi la Polisi kutokukusanyika ama kufanya maandamano katika kipindi hiki cha zoezi la uandikishaji sensa likiendelea hadi hapo litakapomalizika ambapo awali lilipangwa limemalizike Septemba 1, na baadae kuongezwa siku hadi Septemba 8, awali katika makubalino ya CHADEMA na Jeshi la Polisi kabla ya mkutano huo ni kwamba walitakiwa waendelee na mikutano yao.
Kwa mtazamo huu CUF – Chama cha Wananchi tunaona wanaopaswa kubeba lawama hili ni jeshi la Polisi na wala si CHADEMA, kwani kama tulivyoeleza awali ilitosha kuheshimu makubaliano yaliyokuwa yamefanyika baina yao, hata kama kulitokea vurugu haikuhitajika kutumika nguvu kubwa kiasi hiki.
CUF pamoja na kulaani mauaji hayo yanaendelea kutokea lakini pia tunasikitishwa na kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa kwa sababu zinazoweza kuepukika, ili hali kuna uwezekano mkubwa kama busara zingetumika kwa pande zote zinazohusika mauaji kama haya yasingetokea, kwani tunaamini katika vurugu kama hizo zilizotokea hakuna zoezi lolote la sensa lililoendelea kufanyika katika maeneo hayo husika kwa wakati huo.
Kama hivyo ndivyo ilivyo hakukuwa na ulazima wowote wakuzuia watu kukusanyika au kuandamana, kwani wanaokusanyika na kuandamana sio wote, bado kuna watu watakao bakia katika makazi yao ambao wangetosha kutoa taarifa za ndugu na jamaa zao ambao hawapo au hata kuhesabiwa kwa siku zingine kwani zoezi bado linaendelea, na waandikishaji sensa wangeweza kuendelea na majukumu yao bila hofu wala vitisho juu usalama wa maisha yao kutokana na vurugu, kama ambavyo ilivyotokea.
CUF – Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukilililalamikia jeshi la Polisi kuwa liache kufanya kazi kwa ukada bali lizingatie maadili yake ya kazi ambayo ni kulinda usalama wa raia na mali zake,
matukio kama haya ya jeshi la Polisi yalianza ndani ya chama chetu, ambapo itakumbukwa mauaji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi hilo Januari 26 na 27 mwaka 2001 wakati tulipokuwa tukidai Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Tume Huru ya Uchaguzi na kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2000.
CUF Tunamuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuunda Tume Huru itakayoshirikisha Watetezi wa Haki za Binadamu, Madaktari, Wakuu Jeshi la Polisi na Upelelezi na Wajumbe wengine kutoka vyama vya siasa ili kuchunguza mauaji haya yenye taarifa za kutatanisha, ili kuupata ukweli utakaofanyiwa kazi ya kukomesha mauaji kama haya yasiendelee kutokea, ambayo tunahisi yataendelea kutokea kama hatua madhubuti hazikuchukuliwa.

Prof. Ibrahim H. Lipumba
MWENYEKITI